JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAMISEMI
MKOA WA DODOMA
MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) KIDATO CHA PILI -2021
021 KISWAHILI
MUDA SAA 2: 30
MAAGIZO
· Mtihani huu una sehemu AB,C,D NA E
· Jibu maswali yote
KWA MATUMIZI YA WATAHINIWA TU
www.onlineschoobase.com |
NAMBA YA SWALI |
ALAMA
|
SAINI |
01 |
|
|
02 |
|
|
03 |
|
|
04 |
|
|
05 |
|
|
TOTAL |
|
|
UFAHAMU A: (ALAMA (15)
1. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo
Dalali alianza kumnadi beberu akisema ,haya leo tena jamani sogeeni mjipatie vitu bei nafuu .Oneni mnyama mnono huyu ,shilingi elfu sita na mia tano .Nani atakaye na atalipa shilingi ngapi ? Mzabuni wa kwanza alipandisha bei hadi shilingi elifu saba na miambili .Toka hapo bei ilizidi kupanda vikali ajabu , hatimaye mzabuni wa mwisho alikubali kutoa elfu kumi .
MASWALI
a) Dalali alitaja bei gani kama kianzio cha bei ya beberu
b) Mzabuni wa kwanza alitaka kulipa shilingi ngapi?
c) Eleza haya tena jamani sogeeni .Ina maana gani ?
d) Eleza maana ya maneno yafuatayo -:
(1) dalali
(ii)Zabuni
(iii) Nafuu
e) Andika kichwa cha habari hii
SEHEMU B (ALAMA 15) UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI
2 (a). Kwa kuzingatia matumizi ya Kiswahili sanifu sentensi zifuatazo zinamakosa. Ziandike upya kwa ufasaha
MFANO . Kiti mkubwa amevunjika
kiti kikubwa kimevujika
(i) Chai imeingia Inzi
(ii) anakwenda baba kesho safari
(iii) Humwambiaga lakini hanielewi
(iv) Ng’ombe zangu zimeibiwa
(v) Daktari nina kifua sijalala usiku kucha
(b) Kama lugha isingekuwepo katika jamii ya binadamu unafikiri ni matatizo gani manne ambayo yangetokea
(c) Oanisha orodha A na B ili kujenga dhana sahihi. Onyesha majibu yako kwa kisanduku kama hiki
ORODHA A |
i |
ii |
iii |
iv |
v |
ORODHA B |
|
|
|
|
|
ORODHA A (i) huonyesha mpangilio wa maneno kialifabeti jinsi yanavyoandikwa kutamkwa na maana zake (ii) Lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi iii)Maneno yasiyo sanifu yanayozungumza na kikundi kidogo cha watu (iv) Taaluma inayoshughulikia maumbo au mjengo wa maneno katika tungo (v) Ni Mtindo wa lugha inayozungumzwa kulingana na muktadha na kusudi maalumu
|
ORODHA B A- Tanzu za lugha B. Rejesta C- simo D. Sarufi maumbo E. Misemo F. Mofimu G. Nomino H. Kamusi
|
SEHEMU C. ALAMA 15
SARUFI
3. Bainisha aina ya maneno yaliyopigiwa mstari kwenye tungo zifuatazo kwa kuandika kifupisho cha aina ya maneno kilicho sahihi (T,t, E,V,W,H,U)
i. Ngo’ombe huyu ana matata sana
ii. Kitanda cha kwanza kushoto ndicho alichotandika
iii. Macho yake malegevu
iv. Yule mchezaji aliyeshika tama hajapata zawadi
v. Baba analima lakini kaka amesimama
(b) Chunguza jedwali lifuatalo kwa makini kisha jaza sehemu zilizoachwa wazi
Neno |
Mzizi |
Kauli ya kutendana |
Kauli ya kutendwa |
Kusema |
|
|
|
|
|
Kupigana |
|
Kuomba |
|
Kuombana |
|
|
Andik_ |
|
Kuandikwa |
(c ) Tunga sentensi kwa kutumia vipashio vifuatavyo
i. W+t+N
ii. N+ V + Ts + T+ E
iii. W+Ts+Ts + T+E
iv. N+T+N
v. T
SEHEMU D : ALAMA (40 )
4. (a) Kamilisha methali zifuatazo
i. Kuishi kwingi…………………………..
ii. Mchuma janga …………………………….
iii. Chanda chema ……………………….
iv. Asiyekubali kushindwa ………………….
v. Jambo usilolijua ………………………..
(b) Eleza maana ya istilahi zifuatazo
i. Vina
ii. Hadhira
iii. Fani
iv. Mizani
v. Dhamira
(c ) Fasihi simulizi hujitokeza katika tanzu kuu nne
Taja tanzu hizo na kwa kila tazu taja vipera viwili
TANZU |
VIPERA |
(i) |
(i) |
(ii) |
(ii) |
(iii) |
(iii) |
(iv) |
(iv) |
SEHEMU E (ALAMA 15)
UANDISHI WA INSHA /UTUNGAJI
5. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Tegemeo ,s.L.P 130 Dodoma ,una matatizo ya kiafya ,hivyo unahitaji kwenda kutibiwa hospitali ya mkoa wa Dodoma .Adika barua kwa mkuu wako wa shule kuomba ruhusa ya siku mbili (02) jina lako liwe Juhudi Sabuni .
MWONGOZO WA USAHIHISHAJI
MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA PILI 2021
SOMO LA KISWAHILI
|
1. Swali linamtaka mwanafunzi asome kifungu cha habari kisha ajibu maswali aliyopewa
(a) Dalali alitaka shilingi elfu sita na mia tano kama kianzio cha bei ya Beberu (alama 02)
(b) Mzabuni wa kwanza alitaka kulipa shilingi elfu saba na mia mbili (alama 02)
( c) “Haya tena jamani sogeeni” Inamaana kuwa watu wa kusanyike eneo ambalo mnada wa Beberu unaendelea ili wanunue (alama02)
(d) Maana ya maneno
i. Dalali –mtu anayenadi na kuuza vitu vya mnada ,mnadi
ii. Zabuni – uza kwa kushindania bei
iii. Nafuu – rahisi /nyepesi (alama 02@ 6)
iv. Kichwa cha habari hii ni Mnada (alama 3)
SEHEMU B ALAMA 15
2. UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI
(a) (i) Inzi ameingia kwenye chai
(ii) Baba atakwenda safari kesho (Baba atasafiri kesho )
(iii) huwa namwambia lakini hanielewi
(iv) Ngo’mbe wangu wameibiwa
(v) Ninaumwa kifua daktari ,sijalala usiku kucha (alama 1@= 05)
(b) (i) Watu wasingeweza kupashana habari
(ii) Tusingeweza kutambua hisia
(iii)Kusingekuwa na utambulisho wa jamii
( iv) Tusinge elimika (alama 1@= 05
C
Orodha A |
i |
ii |
iii |
iv |
v |
Orodha B |
H |
A |
C |
D |
B |
(ALAMA 1@= 05)
SEHEMU C (ALAM A 15 ) SARUFI
3. (a) (i) ana- t
(ii) Kwanza kushoto –V
(iii) Yake – V
(iv) Yule – W
(v) Lakini - U (ALAMA 1@ = 05 )
(b)
NENO |
MZIZI |
KAULI YA KUTENDANA |
KAULI YA KUTENDWA |
Kusema |
-sem- |
Kusemana |
Kusemwa |
Kupiga |
-pig- |
Kupigana |
Kupigwa |
Kuomba |
-omb- |
Kuombana |
Kuombwa |
Kuandika |
-Andik- |
Kuandikana |
Kuandikwa |
ALAMA 1@= 05
(C) (i) W+t+N- Mimi ni mwanafunzi
(ii) N+ V+Ts +T+E-Mchezaji hodari alikuwa anacheza uwanjani
(iii) W+ Ts+Ts +T+ E – Yeye alikuwa anataka kwenda sokoni
(iv) N+T+N-Mwanafunzi anasoma kitabu
(v) T- Anasoma ( Alama 1@= 05)
SEHEMU D (ALAMA 40)
4. (a) (i) Kuishi kwingi ni kuona mengi
(ii) Mchuma janga hula na wakwao
(iii) chanda chema huvikwa pete
(iv) Asiyekubali kushindwa si mshindani
(v) Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza
(ALAMA 2@= 10)
(b) (i) Vina - silabi za kati na mwisho zenye kufanana katika kila mstari
(ii) Hadhira – msikilizaji /mpokeaji wa kazi za fasihi
(iii) Fani- Umbo la nje la kazi ya fasihi
(iv) Mizani – Ni idadi ya silabi zilizomo kwenye mstari wa shairi au tenzi
(v) Dhamira –Ni lengo la mtunzi wa kazi ya fasihi (ALAMA 3@= 15
(C )
TANZU |
VIPERA |
(I) Hadithi |
(i) Visasili (ii) Soga |
(ii) Ushairi |
(i) Nyimbo (ii) Mashairi |
(iii) Semi |
(i) Methali (ii) nahau |
(iv) Sanaa za maonesho |
(i) Majigambo (ii) Vichekesho |
ALAMA 3@ =15
5. Mtahiniwa anatakiwa kuzingatia muundo wa uandishi wa barua rasmi
- Anuwani ya mwandikiwa (Shule ya sekondari Tegemeo, s.l.p 130 (alama 2 )
- Dodoma (Alama 01)
- Tarehe (Alama 01)
- Anuwani ya mwandishi (mkuu wa shule (alama 02 )
- Mwanzo wa barua (alama 01)
- Kichwa cha barua (alama 02)
- Kiini cha barua (alama 02 )
- Kimalizio cha barua (alama 01)
- Sahihi na jina (alama 02 )
- Cheo (alama 01 )
MFANO
Shule ya sekondari Tegemeo
s.l.p 130
Dodoma
17/5/2021
Mkuu wa shule
Shule ya sekondari Tegemeo
s.l.p 130 .
Dodoma
Ndg
YAH : OMBI LA RUHUSA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA
Mimi ni mwanafunzi ninayesoma kidato cha pili
Ninaomba ninaomba ruhusa ya siku mbili kuanzia tarehe 17/5/2021 hadi tarehe 19/5/2021 ili niweze kwenda kutibiwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma .
Ninasumbuliwa na tatizo la kujaa gesi tumboni kwa muda sasa.
Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litakubaliwa
Natanguliza shukrani zangu za dhati
J.SABUNI
Juhudi Sabuni
( Kidato cha pili - A)
...
No comments:
Post a Comment